Nawambia, vivyo hivyo kuna furaha mbele ya Malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
NIMESAMEHEWA DHAMBI
ZABURI 32:1-11
Sunday, August 16, 2006
By: Rev. Paul Chisoro
>Dhambi ndiyo sababisho ya huzuni ulizonazo
>Una heri wewe ambaye zoezi la kusamehewa dhambi hufanyika kila wakati
>Hatuwezi kuwa wazuri sana kiasi cha kustahili msamaha wa Mungu
>Kinachohitajika ili upate msamaha ni kuwa na uhusiano na Mungu
>Msamaha ulizaliwa msalabani, Yesu alipokufa akalipa deni lako la dhambi
(A) MAANA YA KUSAMEHEWA DHAMBI
•
Bwana kusitiri (kufunika) dhambi zako na kuzitupilia mbali au kuzizika kikwelikweli (Zaburi 32:1)
• Kutokukuhesabiwa upotovu, kuondolewa mashitaka au
kuachiliwa huru na Bwana (Zaburi 32:2)
• Kutokuwa na udanganyifu, uongo au hila rohoni mwako(Zaburi 32:2)
(B) KWA NINI NISAMEHEWE DHAMBI?
1) Nisiposamehewa dhambi zangu nitapewa mshahara wake au
malipizi. Warumi 6:23 “ Kwa maana mshahara wa dhambi ni
mauti………....”
NB-Haki ya ki-Mungu inalazimika kuwalipa wenye dhambi
mishahara yao au wadaiwe milele na milele(Ufunuo 20:11-15)
2) Nikisamehewa dhambi nitaitwa heri, yaani aliyebarikiwa.
>Zaburi 32:1,2 “Heri”, yaani amebarikiwa kiasi cha kuonewa
wivu, ana bahati njema au ana furaha isiyoneneka,
aliyesamehewa dhambi zake
>Warumi 6:23 “bali zawadi ya bure ya Mungu ni Uzima wa
milele kupitia kuungana na Yesu Kristo Bwana wetu
3) Nahitaji uhusiano mzuri na Mungu wangu.
>I Petro 2:24..Mungu aliweka maovu yangu yote juu ya
Kristo, akawa sadaka ya dhambi
4) Nikisamehewa dhambi, Bwana atanifundisha na kunielekeza
njia nitakayoiendea na atanishauri huku jicho lake likinitazama
(Zab.32:8)
5)Maji makuu ya majaribu yakifurika hayatanifikia(Zaburi 32:6-7)
(C) KWA NJIA GANI NAWEZA KUSAMEHEWA DHAMBI?
1) Nitambue ugumu wa maisha ya kuishi na dhambi
zisizosamehewa.
>Zaburi 32:3-4..maneno haya, mifupa yangu ilichakaa, mkono
wako ulinilemea(wa kutopendezwa nami), na jasho langu
lilikauka hata nikawa kama nchi kavu, hufafanua ugumu
wa maisha wa mtu asiyesamehewa dhambi.
2) Nimjulishe Bwana dhambi zangu bila kumficha.
>Zaburi 32:5“Nimjulishe Bwana dhambi zangu bila kumficha
upotovu wangu na kukiri maasi yangu kikamilifu hadi yote ya
nyuma yasemwe kwake
3) Niombe msamaha wa dhambi.
>Zaburi 32:6-Niombe msamaha huu wakati Bwana anapatikana
na kwa kuzingatia kwamba Yeye ni mwingi wa rehema
NB. Tofautisha kumjulisha Bwana dhambi yako na kuomba
msamaha wa dhambi. Baada ya kumjilisha dhambi zako
inabidi uombe msamaha wa hizo dhambi.
4) Kwa kuwasamehe wengine walionikosea (Luka 11:4)
>Marko 11:25-26…Nisipowasamehe wengine makosa yao ,
Baba wa mbinguni hatanisamehe na mimi dhambi zangu
ZINGATIA-ZABURI 130:3-4
Zaburi 130:3 “ Bwana kama wewe ungehesabu maovu, na
kututendea sawasawa na dhambi zetu, ni
nani angesimama? ”
Zaburi 130:4 “Lakini kwako kuna msamaha (ambao ndio
tunaouhitaji mwanadamu) ili upate kuogopwa
na kuabudiwa”

0 Comments:
Post a Comment
<< Home